Hayo yamedokezwa na Waziri wa Wakfu Misri Sheikh Mokhtar Gomaa ambaye amesema wanaotembelea maonyesho hayo wanaweza kununua tarjuma hizo kwa bei nafuu ambayo imepunguzwa kwa asilimia 50.
Sheikh Gomaa amesema kuchapisha tarjama za Qur’ani Tukufu ni katika majukumu ya wizara hiyo ya kueneza fikra za Kiislamu zenye mitazamo ya wastani ili kukabiliana na wenye misimamo mikali.
Maoneyesho ya 52 ya Vitabu ya Cairo yalianza Juni 30 na yataendelea hadi Julai 15.