Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu Iran (ICRO), kanali hiyo ya YouTube ina video zinazohusu maisha ya Imam Khomeini (MA) kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza.
Kanali hiyo imezinduliwa kwa munasaba wa kumbukumbu yamwaka wa 32 tokea aage dunia Imam Khomeini (MA).
Taarifa hiyo aidha imesema semina kuhusu "Mtindo wa Maisha kwa Mtazamo wa Imam Khomeini (MA)" itarushwa moja kwa moja kupitia kanali hiyo ambayo anwani yake ni www.youtube.com/channel/UCsP3Ax93KJZ4IqCgrZKqvXw