IQNA

Msikiti wa Al Aqsa utakuwa wazi Mwezi wa Ramadhani

21:10 - February 25, 2021
Habari ID: 3473681
TEHRAN (IQNA)- Maeneo yote ya Msikiti wa Al Aqsa mjini Al Quds (Jerusalem) yatakuwa wazi kwa waumini Waislamu kwa ajili ya ibada katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Idara ya Wakfu wa Kiislamu katika mji wa Al Quds imesema Waislamu wanaweza kuswali katika maeneo yote ya msikiti huo katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Aidha idara hiyo imetoa wito kwa waumini wote wazinagita sheria za kiafya za kuzuia maambukizi ya COVID-19.

Aidha Idara ya Wakfu wa Kiislamu katika mji wa Al Quds imetoa wito kwa Wapalestina kujitahidi kupata chanjo ya COVID-19 kabla ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili kuzuia kuenea ugonjwa huo.

Msikiti wa Al Aqsa umefungwa mara kadhaa ili kuzuia maambukizi ya COVID-19.

Waislamu Wapalestina hujitokeza kwa wingi kusali katika Msikiti wa Al Aqsa ili kuulinda mkabala wa njama za Wazayuni wanaotaka Kuuyahudisha.

Katika miaka ya hivi karibuni, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshadidisha hujuma na uvamizi wake dhidi ya maeneo ya Wapalestina ukifanya njama za kufikia malengo yake haramu katika ardhi za Wapalestina.

Msikiti wa al-Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu umekuwa ukiandamwa na njama mtawalia za utawala vamizi wa Israel, hatua ambazo zinakwenda sambamba na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina.

 

3955964  

Kishikizo: aqsa ramadhani palestina
captcha