IQNA

Wabahrain wanaadhimisha mwaka wa 10 wa mwamko dhidi ya utawala wa Aal Khalifa

20:36 - February 12, 2021
Habari ID: 3473644
TEHRAN (IQNA) - Wakati ukikaribia mwaka wa 10 tokea uanze mwamko wa wananchi wa Bahrain dhidi ya utawala wa ukoo wa Aal Khalifa nchini humo, utawala huo dhalimu umeshadidisha ukandamizaji na utumiaji mabavu dhidi ya wananchi wanaotaka mabadiliko.

Katika kipindi hiki wananchi wa Bahrain wameanzisha harakati katika mitandao ya kijamii yenye hashtegi ya #ثبات_حتی_النصر_۱۰ yaani ‘kusimama kidete hadi mwaka wa kumi wa ushindi’

Mwamako wa watu wa Bahrain dhidi ya utawala wa kifalme ulianza Februari 14 2011. Mwamko huu ni tofauti na harakati zingine za mwamko katika uliwengu wa Kiarabu ukiwemo mwamko uliopelekea kuangushwa Zine El Abidine Ben Ali wa Tunisia au Husni Mubarak wa Misri. Tofauti ya mwamko wa watu wa Bahrain ni kuwa, nchi hiyo inapakana na Saudi Arabia ambayo ni mpinzani na adui mkubwa zaidi wa mwamko na mapinduzi ya wananchi katika nchi za Kiarabu.

Kwa msingi huo, mwezi mmoja baada ya kuanza mwamko wa Februari 14, utawala wa Saudia ulituma wanajeshi wake Bahrain kwa lengo la kuwakandamiza raia wa nchi hiyo. Askari hao vamizi wa Saudia waliingia Bahrain katika fremu ya 'Ngao ya Kisiwa' ya Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi. 'Ngao ya Kisiwa' ni mapatano ya ushirikiano wa kijeshi wa nchi za Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi kwa lengo la kukabiliana na hujuma ya kigeni.

Hivi sasa ukiwa ni mwaka wa 10 tokea uanze mwamko wa watu wa Bahrain, wanajeshi wa Saudia na pia wale wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) bado wako nchini Bahrain na wanashirikiana na askari waliokodiwa wa utawala wa ukoo wa Aal Khalifa katika kuwakandamiza wananchi ambao wamekuwa wakiandamana kupigania mageuzi hasa ya kutaka kuwepo utawala unaochaguliwa moja kwa moja na wananchi.

پویش مجازی گرامیداشت دهمین سالگرد انقلاب بحرین

Wabahrain pia hivi sasa wanaadhimisha mwaka wa 10 wa mwamko wao wakati ambao mwaka jana utawala wa Aal Khalifa ulitangaza rasmi kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala wa Kizayuni wa Israel. Bahrain na UAE mnamo Septemba 15 mwaka 2020 ziliafiki kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Uhusiano wa Manama na Tel Aviv ulikuwa wa siri lakini ulitangazwa rasmi mwaka jana ambapo Oktoba 2020, Waziri wa Mambo ya Nje wa Bahrain alitembelea Israel.  Wananchi waliowengi Bahrain wanapinga vikali uanzishwaji uhusiano wa aina yoyote ile baina ya nchi yao na Israel. Hivi sasa katika wakati wa kukaribia mwaka wa 10 wa mwamko wa Februari 14, wananchi wa Bahrain wanapanga kushiriki katika maandamano ambayo mbali na kutaka mageuzi ya mfumo wa utawala pia watabainisha upinzani wao mkubwa kwa hatua ya kuanzishwa uhusiano na utawala haramu wa Israel.

3953584

captcha