IQNA

Kiongozi Muadhamu atangaza sera juma za kulinda mazingira Iran

13:29 - November 19, 2015
Habari ID: 3454537
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma Sayyed Ali Khamenei ametangaza sera jumla kuhusiana na kulinda mazingira nchini Iran.

Kati ya nukta ambazo Kiongozi Muadhamu alitilia mkazo katika sera hizo zilizotangazwa Jumanne na ambazo zinapaswa kutekelezwa na mihimili mitatu ya dola ni pamoja na kubuniwa mfumo endelevu wa kulinda mazingira nchini.

Aidha sera hizo pia zinajumuisha kusimamiwa kwa utaratibu mazingira, kufanya kuwa kosa la jinai uharibifu wa mazingira, na kuwekwa sera rasmi zinazoenda sambamba na ulindaji mazingira.

Kiongozi Muadhamu pia alisisitiza kuhusu ulazima wa kuunda uchumi wa kijani au uchumi unaozingatia kulindwa mazingira ikiwa ni pamoja na kupunguza gesi za sumu viwandani, nishati safi, kilimo kisichotegemea mada za kemikali na usimamizi bora wa vyanzo vya maji nchini Iran.

Halikadhalika Kiongozi Muadhamu alisisitiza umuhimu wa kukabiliana na uchafuzi wa hewa na maji.

3453636

 

captcha