IQNA

Kiongozi wa Kiislamu Senegal atangaza Jihadi ya Kijani

10:37 - August 13, 2015
Habari ID: 3341790
Kiongozi wa Kiislamu wa nchini Senegal ametaka kutekelezwa “Jihadi ya Kijani” dhidi ya uchafuzi wa mazingira, akiliomba bunge la nchi hiyo na pia jamii nzima ya Waislamu kushiriki katika kile alichokiita jukumu la wazi la Kiislamu la kulinda mazingira.

. Imam Youssoupha Sarr amesema kwenye mahojiano Jumapili hii na kanali ya lugha ya Kiingereza ya al Jazeera kuwa: Haamini kuona jinsi watu wa taifa hilo la Kiislamu analotoka walivyozoea kuishi katika mazingira yaliyochafuliwa na mifuko ya plastiki na aina nyingine za uchafu. Imam Sarr ameongeza kuwa: Dini ya Kiislamu imebainisha wazi kuhusu suala la mazingira, na kwamba aina yoyote ya uchafuzi au uharibifu wa mazingira ni dhambi na imekatazwa waziwazi. Imam Youssoupha Sarr wa Senegal amesema kuwa watu wanapasa kukumbushwa juu ya suala hili. Kiongozi huyo wa Kiislamu amesema anaamini kuwa Mwenyezi Mungu amewaruzuku wanadamu mazingira asilia na kwa msingi huo jamii ya mwanadamu ina jukumu la kuyalinda kwa gharama yoyote ile.../mh

3341608

captcha