IQNA

Kikao cha ‘Misimamo Wastani ya Kidni’ kufanyika nchini Uganda

18:35 - June 12, 2015
Habari ID: 3313360
Uganda itakuwa mwenyeji wa kikao cha kwanza cha kitaalamu kuhusu ‘Nafasi ya Misimamo ya Wastani ya Kidini Katika Kufikia Ulimwengu Usio na Machafuko’.

Kwa mujibu wa Idara ya Habari ya Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu Iran (ICRO), kikao hicho kitafanyika tarehe 16 Juni mjini Kampala Uganda kwa ushirikiano wa Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Uganda , Chuo Kikuu cha Kampala na Baraza la Kidini Uganda.
Kikao hicho kinatazamiwa kuhudhuriwa na washiriki 30 wakiwemo viongozi wa kidini, wasomi wa vyuo vikuu na wanaharakati wa mazungumzo ya kidini wakiwemo Waislamu, Wakristo,  Mayahudi, Wahindu na Mabuddha.
Imearifiwa kuwa kikao hicho cha kwanza cha ‘Nafasi ya Misimamo ya Wastani ya Kidini Katika Kufikia Ulimwengu Usio na Machafuko’ kinatazamiwa kumalizika alasiri kwa kutolewa taarifa ya mwisho na pia kwa hotuba ya Balozi wa Iran nchini Uganda.../mh

3313320

captcha