IQNA

Maonyesho ya Qur'ani

Kitengo cha Hijabu katika Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran kuwavutia wengi

14:49 - March 19, 2024
Habari ID: 3478540
IQNA - Mkuu wa sehemu ya Hijabu na Ifaf ya Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran ameleeza kuwa ni moja ya sehemu zinazotembelewa zaidi katika maonyesho hayo ya kila mwaka.

Assadollah Soleimani aliiambia IQNA kwamba sehemu ya Hijabu na Ifaf imekuwa sehemu ya maonyesho kwa miaka 18.

Mwaka huu, wazalishaji 400 wa bidhaa za Hijabu na Ifaf wamejiandikisha kuonesha bidhaa zao, alisema, akisikitika kuwa kutokana na ufinyu wa nafasi, ni mabanda 150 pekee yanapatikana katika sehemu hiyo, ambayo iko upande wa Magharibi wa  Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini (RA) ambao utakuwa mwenyeji wa maonyesho hayo.

Alitumai kwamba kwa msaada wa Naibu Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu anayesimamia masuala ya Qur'ani Etrat angalau mabanda 100 zaidi yataongezwa kwenye sehemu hiyo katika siku zinazofuata.

 

Wanaotembelea sehemu ya Hijabu na Ifaf wanaweza kununua Hijabu na bidhaa zote zinazohusiana na vazi hilo la staha la Kiislamu.

Kitengo hicho kinalenga kuwasilisha utamaduni wa Hijabu unaotokana na mafundisho ya Qur'ani Tukufu, Mtume Muahmmad (SAW) na Ahl-ul-Bayt (AS).

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran kila mwaka huandaliwa na Wizara ya Utamaduni na Muongozo ya Kiislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Maonyesho hayo yanalenga kukuza dhana za Qur'ani na kuendeleza shughuli za Qur'ani.

Huwasilisha pia mafanikio ya hivi punde zaidi yanayohusiana na Qur'ani nchini Oram na pia bidhaa mbalimbali zinazotolewa kwa ajili ya kutangaza Kitabu hicho Kitakatifu.

Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini (RA)  unatazamiwa kuwa mwenyeji wa toleo la 31 la tukio la Qur'ani kuanzia Machi 20 hadi Aprili 2.

Kama toleo lililopita, maonyesho ya mwaka huu yatafanyika yenye kauli mbiu "Nilikusoma" ikiwa ni kuashiria usomaji wa Qur'ani Tukufu.

3487603

Habari zinazohusiana
captcha