IQNA

Maandamano Ulimwenguni Kote ya Kuunga mkono Palestina kwa Mashambulizi na Mauaji ya kikatili Yanayofanywa ya Israel dhidi ya Gaza

TEHRAN (IQNA) – Mamilioni ya watu kote duniani walijitokeza mitaani Oktoba 20 kushutumu kuendelea kwa mashambulizi ya kikatili ya Israel dhidi ya Gaza ambayo yamesababisha zaidi ya Wapalestina 4,100 kuuawa ndani ya wiki mbili.

Maandamano makubwa ya kuunga mkono Palestina na kulaani utawala wa Israel yalienea katika nchi nyingi zenye Waislamu wengi baada ya swala ya Ijumaa.

Mikutano ya hadhara iliripotiwa nchini Iran, Uturuki, Misri, Jordan, Lebanon, Syria, Qatar, Iraq, Yemen, Malaysia na maeneo mengine, katika miji zaidi ya moja katika baadhi ya nchi kwa maandamano makubwa .

 

3485672