IQNA

Kiongozi Muadhamu

Hatua ya Bunge ya la Iran kukabiliana na vikwazo ilizuia mkanganyiko katika suala la nyuklia

21:13 - May 24, 2023
Habari ID: 3477038
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amasema sheria ya kistratijia iliyopitishwa na Bunge la Iran mwaka 2020 ili kukabiliana na vikwazo iliiokoa nchi kutokana na "kuchanganyikiwa katika suala la nyuklia".

Ayatullah Khamenei ambaye mapema leo Jumatano amehutubia kikao cha wabunge waliokwenda kuonana naye mjini Tehran, amepongeza sheria za kistratijia zilizopitishwa na Bunge, ukiwemo Mpango wa Kimkakati wa Kukabiliana na Vikwazo.

Amesisitiza kuwa: "Sheria ya hatua za kimkakati iliokoa nchi kutokana na kuchanganyikiwa katika suala la nyuklia," na kusema, sheria hiyo ilifafanua wazi kile tunachopaswa kufanya na tunashuhudia matokeo yake ulimwenguni."

Chini ya sheria hiyo, iliyoidhinishwa Disemba 2020, serikali ya Iran inatakiwa kuzuia ukaguzi wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) katika miradi yake ya kuzalisha nishati ya nyuklia na kuharakisha maendeleo ya miradi ya nyuklia ya nchi, zaidi ya mipaka iliyowekwa chini ya makubaliano ya nyuklia ya 2015.

Sheria hiyo ilipitishwa kwa nia ya kukabiliana na vikwazo haramu vilivyowekwa na Marekani na washirika wake wa Magharibi dhidi ya Iran.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekutaja kutambua matatizo ya nchi na kutunga sheria za kutatua matatizo hayo kuwa ni miongoni mwa sifa za Bunge la 11 na kuongeza kuwa: Sheria nyingi za kupambana na rushwa, kuondoa ubaguzi, kuondoa ukiritimba na kuboresha mazingira ya biashara zimeidhinishwa na Bunge.

Mwanzoni mwa hotuba yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelipongeza taifa kubwa la Iran kwa mnasaba wa tarehe 3 Khordad, siku ya kumbukumbu ya kukombolewa mji wa Khorramshahr. Amewaasa wananchi wote kusoma vitabu vilivyoandikwa kuhusu operesheni ya kijeshi ya kuukomboa mji huo iliyopewa jina la Operesheni ya Kuelekea Baitul Muqaddas wakati wa vita vya kulazimishwa vilivyoanzishwa na dikteta wa zamani wa Iraq, Saddam Hussein, dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na kusema: Muhimu zaidi kuliko ushindi huu mkubwa ni ubunifu, mipango ya vita inayoweza kufundishwa katika vyuo vikuu vya vita, kujitolea mhanga, ushujaa uliokuwa juu ya uwezo wa wanadamu wa kawaida, mashahidi wa daraja la juu, na mambo mengine ya aina yake yaliyoshuhudiwa ndani ya operesheni hiyo ambayo hayapaswi kuachwa yafifie au kusahaulika.

Mji wa Khorramshahr ulioko katika mkoa wa Khozestan Kusini Magharibi mwa Iran ulikombolewa na wapiganaji wa Kiislamu kutoka kwenye udhibiti wa majeshi vamizi ya Iraq katika siku kama hii ya leo. Mji huo ulikuwa chini ya uvamizi wa majeshi ya Iraq kwa muda wa karibu mwaka mmoja na miezi minane. Uvamizi dhidi ya mji huo ulijiri mwanzoni mwa vita vya miaka minane vya kulazimishwa. Siku hii inajulikana katika utamaduni wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kuwa, "Siku ya Muqawama na Ushindi". 

/4143070

Habari zinazohusiana
captcha