Adhana ni wito wa Kiislamu wa kutangaza kwamba umefika wakati wa Sala maalum ya faradhi ya kila siku.
Klipu hiyo lilisambaa 'kupendwa' mara 7000 na kutumwa tena mara 1000 baada ya muda mfupi. Wafuasi wengi wa Winter walishiriki kuvutiwa na sauti nzuri ya Adhana.
Inafurahisha, Henry Winter ni kaka wa Skeikh Abdal Hakim Murad, mkuu wa Chuo cha Waislamu cha Cambridge.
Abdal Hakim, ambaye zamani kabla ya kusilimu alikuwa Timothy John Winter, ni msomi wa Kiingereza, mwanatheolojia na mwanazuoni wa Kiislamu ambaye alisilimu mnamo 1979.
Saa chache kabla ya kuzinduliwa kwa Kombe la Dunia 2022, Qatar ilizindua mipango kadhaa ya kutambulisha Uislamu kwa wageni wakati wa mashindano hayo ya soka ya kimataifa.
Kwa mfano, katika katika vyumba vya wageni vya hoteli za Qatar kuna QR Code ambayo inatoa maelezo kwa wageni kuhusu Uislamu na utamaduni wa Qatar katika lugha zote.
Qatar pia imeweka maandishi makubwa kote nchini humo yenye hadith za Mtume Muhammad (SAW) ili kutambulisha Uislamu kwa mashabiki wanaokuja wa Kombe la Dunia.
Kwingineko, mashabiki waliosafiri kuelekea Qatar kwa ajili ya Kutazama Kombe la Dunia la 2022, hawataruhusiwa kunywa pombe viwanjani.