IQNA

Harakati za Qur'ani

Wanafunzi 150,000 wajiandikisha kwa kozi ya Qur'ani nchini Jordan

15:16 - August 29, 2022
Habari ID: 3475700
TEHRAN (IQNA)- TEHRAN (IQNA) - Kozi za kuhifadhi Qur'ani katika vituo vya Qur'ani vya Jordan zimekaribishwa kwa furaha na wanafunzi wa shule Wizara ya Wakfu ilisema.

Waziri wa Wakfu wa Jordan Mohammad al-Khalaileh alisema zaidi ya wanafunzi 150,000 wamesajili majina yao kuchukua kozi hizo.

Alisema wavulana na wasichana wa rika tofauti wamejiandikisha kuhifadhi Qur'ani Tukufu, tovuti ya al-Ghad iliripoti.

Kulingana na Khalaileh, wanafunzi wenye ulemavu wa macho hujifunza Quran kwa moyo pamoja na wanafunzi wengine mwaka huu.

Amesisitiza haja ya kulea kizazi cha Qur'ani kwa kuwahimiza wanafunzi kushiriki katika shughuli za Qur'ani.

Ameyasema hayo katika hafla iliyofanyika kuashiria kuhitimishwa kwa mafunzo ya Qur'ani majira ya kiangazi.

Afisa huyo pia alirejelea kupangwa kwa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya nchi hiyo na kusema Jordan ni moja ya mataifa ya kwanza ya Kiislamu ambayo yalianza tena kufanya mashindano yake ya kimataifa ya Qur'ani baada ya kusimamishwa kutokana na janga la coronavirus.

Aidha ameashiria juhudi za Wizara ya Wakfu za kukuza shughuli za Qur'ani, ikiwa ni pamoja na kuchapisha nakala za Qur'ani na kuandaa programu za Qur'ani katika ngazi za kitaifa na kimataifa.

Kila mtu pia anapaswa kuongozwa na Kitabu cha Mwenyezi Mungu katika mwenendo wake, tabia na maneno yake, aliendelea kusema.

4081417

 

captcha