IQNA

Misri yaanza ujenzi wa Msikiti wenye uwezo wa kubeba waumini laki

21:12 - March 14, 2021
Habari ID: 3473734
TEHRAN (IQNA)- Misri imeanza kujenga kituo cha utamaduni wa Kiislamu ambacho kitajumuisha msikiti mkubwa.

Kwa mujibu wa taarifa msikitu huo utajulikana kama “Msikiti wa Misri’ na utakuwa na uwezo wa kubeba waumini 107,000 baada ya ujenzi wake kukamilika.

Mahmoud Abbas mmoja kati ya wahandisi wanaohusika na mradi huo amesema msikiti huo utakuwa na minara yenye urefu wa mita 140.

Halikadhalika pembizoni mwa msikiti huo kutakuwa na kumbu kadhaa za mijimuiko ya kidini na sherehe pamoja na vituo vya kutoa mafunzo ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu kwa wanaume, wanawake na watoto.

Msikiti huo unajengwa katika mji mpya unaojengwa nje ya mji mkuu wa Misri Cairo ambao ujenzi wake ulianza mwaka 2015.

3959520

Kishikizo: misri msikiti
captcha