Aidha, Amina Ahmad wa Jimbo la Borno ametangazwa mshindi katika kitengo cha wanawake katika mashindano hayo ya kitaifa.
Dkt. Sani Yunus Birnin-Tudu, mratibu wa kitaifa wa mashindano' alitangaza matokeo hayo siku ya Jumamosi na kusema washiriki walishindana katika kuhifadhi Qur'ani kikamilifu. Aidha aliongeza kuwa mashindano hayo yaliwajumuisha washiriki 360 kutoka majimbo 32 ya Nigeria na yaliendelea kwa muda wa wiki moja.
Dkt. Birnin-Tudu amesema washindi wamatunukiwa zawadi mbali mbali kama vile magari mapya, Qur'ani za kidijitali, laptopu na fedha taslimu.
Akizungumza katika hafla hiyo Profesa Abdullahi Zuru Mkuu wa Chuo Kikuu cha Usmanu Danfodio cha Sokoto, ambacho kiliandaa mashindano hayo, amepongeza Serikali ya Jimbo la Katsina kwa kuwa kuwa mwenyeji wa mashindano hayo ambayo yalifana.