IQNA

Mwanamke Muislamu kuwania Urais Russia, anatumai kumshinda Putin

11:26 - January 01, 2018
Habari ID: 3471335
TEHRAN, (IQNA)-Mwanamke Muislamu, Aina Gamzatova, ametangaza kujitosa katika uchaguzi wa urais wa Russia Machi 2018 kwa lengo la kumuondoa madarakani Rais Vladimir Putin wa nchi hiyo.

Bi. Gamzatova mwenye umri wa miaka 46 kutoka Jamhuri ya Dagehstan katika Shirikiso la Russia alitangaza uamuzi wake Jumamosi mbele ya mamia ya wafuasi akiwa Makhachkala, mji mkuu wa Daghestan.

Bi.Gamzatova anaongza shirika kubwa zaidi la vyombo vya habari vya Waislamu Russia lijulikanalo kama-Islam.ru. shirika hilo lina miliki televisheni, radio na taasisi za uchapishaji  vitabu vya Kiislamu na pia lina kitengo cha misaada. Mume wa Bi. Gamzatova ni Sheikh Ahmad Abdulaev ambayo ni mufti wa Jamhuri ya Dagehstan ambayo ni kati ya maeneo yenye Waislamu wengi nchini Russia.

Halikadhalika kiitikadi, Bi. Gamzatov ni mfuasi wa Tariqa yenye maelfu ya wafuasi na kiongozi wake alikuwa ni Said-Afandi Chirkavi ambaye aliuawa shahidi katika hujuma ya kigaidi eneo la  Caucasus  mwaka 2012.

Aidha mume wa kwanza wa Bi. Gamzatova  aliyekuwa kiongozi wa Waislamu, Said Muhammad Abubakarov, aliuawa katika hujuma ya magaidi wakufurishaji mwaka 1998.

Uamuzi wa Bi. Gamzatova kuwania urais ni gumzo miongoni mwa jamii ya Waislamu Russia ambapo baadhi wanamuunga mkono huku wengine wakimpinga wakisisitiza kuwa Rais Putin anapaswa kuendelea kutawala. Pia kuna wale wanaosema kwa yakini kuwa hataweza kushindi lakini kugombea kwake kutaimarisha taswira ya wanawake Waisalmu nchini Russia hasa kutokana na kuwa anazingatia vazi la Hijabu.

captcha