IQNA

Maandamano London, New York kulaani mauaji ya Waislamu Nigeria

0:16 - December 20, 2015
Habari ID: 3467081
Maandamano ya kulaani mauaji ya umati ya Waislamu nchini Nigeria yameendelea kushuhudiwa katika pembe mbali mbali za dunia.

Kundi kubwa la waandamanaji limekusanyika nje ya ubalozi wa Nigeria katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York nchini Marekani kulaani ukatili wa jeshi la Nigeria dhidi ya Waislamu. Aidha waandamanaji wamesisitiza kuhusu kuachiwa huru kiongozi wa kidini Sheikh Ibrahim Zakzaky na mke wake.
Maandamano mengine ya kulaani mauaji ya Waislamu wasio na hatia nchini Nigeria yameshuhudiwa katika miji tofauti ya Uingereza.
Siku ya Ijumaa maelfu ya watu walifanya maandamano nchini Iran kulaani mauaji hayo. Waandamanaji hao waliowashirikisha watu wa matabaka mbalimbali walitoa nara za kuchukizwa mno na jinai hiyo na kubeba mabango yaliyoakisi hasira na chuki ya Waislamu kote dunia dhidi ya mabeberu wa kimataifa hususan Marekani na Israel.
Maandamano kama hayo ya kulaani mauaji yaliyofanywa na jeshi la Nigeria dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia katika mji wa Zaria pia yamefanyika katika miji yote mikubwa nchini Iran. Miji mbalimbali ya Nigeria kadhalika hapo jana ilishuhudia maandamano makubwa ya Waislamu waliokuwa wakilaani mauaji hayo.
Usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita, jeshi la Nigeria liliishambulia Husainiyyah ya Baqiyyatullah katika mji wa Zaria pamoja na nyumba ya Sheikh Zakzaky na kuwaua mamia ya Waislamu kwa kisingizio kwamba Harakati ya Kiislamu ya Nigeria ilikula njama ya kutaka kumuua kamanda wa jeshi na kufunga njia kwa ajili ya shughuli za mijumuiko ya harakati hiyo. Baadhi ya ripoti zinasema kuwa, idadi ya waliouawa katika shambulio hilo la jeshi la Nigeria inafikia elfu moja.
Ikumbukwe kuwa, kwa kutoa tuhuma kwamba Harakati ya Kiislamu ya Nigeria ilikula njama ya kutaka kumuua kamanda wa jeshi na kufunga njia kwa ajili ya shughuli za mijumuiko ya harakati hiyo, Jumamosi iliyopita, jeshi la Nigeria liliishambulia Husainiyyah ya Baqiyyatullah katika mji wa Zaria na siku ya Jumapili likahujumu nyumba ya Sheikh Ibrahim Zakzaky na kuwaua mamia ya Waislamu.
Kuhusu idadi ya watu waliouawa, Nusaibah Zakzaky, binti wa Sheikh Ibrahim Zakzaky amesema watu wapatao 450 waliuawa huko Zaria na maiti zipatazo 300 ziko hospitalini, na hivyo idadi kamili ya waliouawa inaweza kupindukia watu 1000.

3467004

captcha