IQNA

Maandamano duniani kulaani mauaji ya Waislamu Nigeria

21:00 - December 18, 2015
Habari ID: 3465571
Maandamano yamefanyika katiak maeneo mbali mbali duniani ikiwa ni pamoja na Iraq, Bahrain, Uingereza na Pakistan kulaani mauaji ya Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Nigeria.

Maelfu ya watu wamefanya maandamano leo kote nchini Iran kulaani mauaji yaliyofanywa siku chache zilizopita na jeshi la Nigeria dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia katika mji wa Zaria nchini Nigeria.
Mjini Tehran maandamano hayo mjini Tehran yamefanyika baada ya Swala ya Ijumaa ambao washiriki walaani vikali mauaji ya Waislamu hao wa Nigeria wakisema ni jinai dhidi ya binadamu.
Waandamanaji hao waliowashirikisha watu wa tabaka mbalimbali wametoa nara za kuchukizwa mno na jinai hiyo na kubeba mabango yaliyoakisi hasira na chuki ya Waislamu kote dunia dhidi ya mabeberu wa kimataifa hususan Marekani na Israel.
Waandamanaji mjini Tehran pia wamekemea kimya cha jamii ya kimataifa mbele ya jinai ya mauaji ya Waislamu wa Nigeria ambao daima wamekuwa mstari wa mbele kuwatetea watu wanaokandamizwa wa Palestina.
Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami  ameashiria mauaji ya Waislamu wa Kishia nchini Nigeria yaliyofanywa na jeshi la nchi hiyo na kulaani mauaji mauaji hayo. Vilevile amewaonya watekeleza wa mauaji hayo pamoja na serikali ya Nigeria kwamba, tukio hilo litakuwa na matokeo ya majuto. Ayatullah Khatami ameeleza kuwa, matukio kama hayo yanafanyika kwa matakwa ya utawala wa Kizayuni wa Israel, Mawahabi na makundi ya kigaidi kama Daesh na Boko Haram.
Amesema serikali ya Nigeria inapaswa kuchukua hatua za haraka kuhakikisha kwamba, waliohusika na jinai hiyo wanapandishwa kizimbani na wakati huo huo kuzuia kukaririwa matukio kama hayo.
Maandamano pia yamefanyika katika maeneo mbali mbali ya Nigeria kulaani kuuawa kwa umati Waisalmu zaidi ya elfu moja na jeshi la nchi hiyo. Maandamano makubwa yamefanyika katika miji ya Bauchi, Katsina na Gambi kaskazini mwa Nigeria.
Ikumbukwe kuwa, kwa kutoa tuhuma kwamba Harakati ya Kiislamu ya Nigeria ilikula njama ya kutaka kumuua kamanda wa jeshi na kufunga njia kwa ajili ya shughuli za mijumuiko ya harakati hiyo, Jumamosi iliyopita, jeshi la Nigeria liliishambulia Husainiyyah ya Baqiyyatullah katika mji wa Zaria na siku ya Jumapili likahujumu nyumba ya Sheikh Ibrahim Zakzaky na kuwaua mamia ya Waislamu.
Kuhusu idadi ya watu waliouawa, Nusaibah Zakzaky, binti wa Sheikh Ibrahim Zakzaky amesema watu wapatao 450 waliuawa huko Zaria na maiti zipatazo 300 ziko hospitalini, na hivyo idadi kamili ya waliouawa inaweza kufikia watu 1000.

3465552

captcha