IQNA

Mwana wa Allamah Zakzakay:Hatima ya baba haijulikani

19:58 - December 18, 2015
Habari ID: 3465562
Mwana wa kiume wa Sheikh Ibrahim Zakzaky wa nchini Nigeria amesema familia bado haijazungumza na kiongozi huyo wa Waislamu wa madhehebu ya Shia tangu alipokamatwa na kwa mantiki hiyo hawana uthibitisho wowote kama yuko hai au la.

Kijana huyo pia amesema familia haijaweza kupata taarifa yoyote kutoka kwa jeshi la Nigeria kuhisiana na hali ya Sheikh Ibrahim Zakzaky. Familio ya kiongozi huyo wa Kiislamu imetaka serikali kuruhusu daktari wa kujitegemea kukutana na Sheikh Zakzaky na kisha kutoa taarifa isiyopendelea upande wowote kuhusiana na hali yake.

Ikumbukwe kuwa, kwa kutoa tuhuma kwamba Harakati ya Kiislamu ya Nigeria ilikula njama ya kutaka kumuua kamanda wa jeshi na kufunga njia kwa ajili ya shughuli za mijumuiko ya harakati hiyo, Jumamosi iliyopita, jeshi la Nigeria liliishambulia Husainiyyah ya Baqiyyatullah katika mji wa Zaria na siku ya Jumapili likahujumu nyumba ya Sheikh Ibrahim Zakzaky na kuwaua mamia ya Waislamu.

Kuhusu idadi ya watu waliouawa, Nusaibah Zakzaky, binti wa Sheikh Ibrahim Zakzaky amesema watu wapatao 450 waliuawa huko Zaria na maiti zipatazo 300 ziko hospitalini, na hivyo idadi kamili ya waliouawa inaweza kufikia watu 1000.

Wanaharakati wa Nigeria wameripoti kuwa maiti za Waislamu waliouawa katika maafa ya Zaria kaskazini mwa nchi hiyo zinachomwa moto na kuzikwa kwenye makaburi ya halaiki.

Wanaharakati hao wamefafanua kuwa serikali na jeshi la Nigeria zimezika maiti za Waislamu kwenye makaburi ya halaiki na kuzichoma moto baadhi ya nyengine ili kufuta ushahidi wa jinai ziliyotenda katika maafa ya Zaria.

3465460

captcha