IQNA

Trump: Israel inawasaidia magaidi wa ISIS (Daesh)

14:41 - December 16, 2015
Habari ID: 3463979
Donald Trump, mwanasiasa wa chama cha Republicans amesema baadhi ya waitifaki wa Marekani, ikiwemo Israel, wanaliunga mkono na kulipa misaada kundi la kigaidi la ISIS au Daesh.

Huku akiunyooshea kidole cha lawama utawala haramu wa Israel kwa njia isiyo ya moja kwa moja, mwanasiasa huyo amesema waitifaki ambao Marekani inawalinda kijeshi na kisiasa wanatoa mabilioni ya dola kwa makundi ya kigaidi kama ISIS na al-Qaeda. Trump amesema serikali ya Rais Barack Obama inajua vyema kuhusu uungaji mkono wa Israel kwa makundi ya kigaidi lakini imeendelea kubakia kimya. "Wale tunaowaita waitifaki wetu ambao tunafanya nao kazi na tunawalinda kijeshi na hata kisiasa, ndio hao hao wanaowapa magaidi wa Daesh na al-Qaeda pesa nyingi" amesema mwanasiasa huyo bilionea wa chama cha Republicans anayetafuta tiketi ya chama hicho kwa ajili ya kuwania urais mwaka ujao nchini Marekani
Trump ambaye alitarajiwa kuitembelea Israel Disemba 28 ametangaza kufuta safari hiyo ingawa hakutoa sababu za hatua yake hiyo.
Siku chache zilizopita, Donald Trump aliitaka ikulu ya White House kupiga marufuku Waislamu kuingia nchini Marekani kwa sababu ya eti kudhibiti ugaidi. Matamshi hayo yaliamsha hasira za Waislamu kote duniani. Wanasiasa 14 wanawania tiketi ya chama cha Republicans kwa ajili ya kuwania urais mwaka ujao.

3463605

captcha