IQNA

Askari wa Utawala wa Kizayuni waua Wapalestina wawili

14:32 - December 16, 2015
Habari ID: 3463972
Wapalestina wengine wawili wameuawa shahidi katika hujuma za wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wasio na hatia.

Vijana hao kwa majina ya Ahmad Hassan Jahjouh na Hekmat Hamdan leo wameuawa shahidi kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa Kizayuni katika kambi ya Kalandiya Quds Kaskazini.

Kwingineko watu wengine 22 wamekamatwa na wanajeshi wa Kizayuni akiwemo binti mdogo katika eneo hilo.

Kufuatia kuongozeka ukatili wa utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina, uchunguzi wa maoni uliofanyika hivi karibuni umebaini kuwa zaidi ya asilimia 75 ya Wapalestina wanaunga mkono Intifahda ya Tatu au mwamko dhidi ya Wazayuni.

Machafuko mapya katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu yalianza baada ya utawala haramu wa Israel kuwazuia Waislamu wa Palestina kuingia katika Msikiti Mtakatifu wa al Aqsa mwezi Agosti mwaka huu.

Wapalestina zaidi ya 120 wakiwemo wanawake na watoto wameuawa kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa Israel tokea mwanzo wa mwezi wa Oktoba, ilipoanza Intifadha ya tatu.

3463841

captcha