Carolyn Walker-Diallo ameapishwa kuwa jaji katika mahakama moja ya Wilaya ya Manispaa ya 7, katika jimbo la Brooklyn, baada ya kuteuliwa mwezi uliopita.
Diallo anakuwa mwanamke wa kwanza mwenye asili ya Afrika kuapishwa kuwa jaji nchini Marekani kwa kutumia Qurani.
Itakumbukwa kuwa, mwanamke wa kwanza Muislamu kuapishwa kuwa jaji nchini Marekani alikuwa Sheila Abdu-Salaam, katika mahakama ya juu ya New York, mwaka 1992.
Mwanamke mwingine Muislamu mwenye asili ya Kiarabu, Chalene Mekled Elder, aliajiriwa katika mahakama ya 3rd Circuit, jimboni Michigan mwaka 2006.
"Alhamdulillah, ni kwa unyeneyekvu mkubwa nakubali jukumu hili nzito kutoka kwa jamii yangu. Nitahakikisha kuwa kila mtu anapata uadilifu mahakamani," Walker ameandika katika tovuti yake.