IQNA

Turathi ya Kiislamu

Urejeshaji wa Msahafu wa Karne 5 huko Taiwan

18:39 - June 07, 2023
Habari ID: 3477116
Urejeshaji wa Msahafu (Qur'ani Tukufu) ulioandikwa miaka 500 iliyopita hivi karibuni umekamilika eneo la China laTaiwan .

Msahafu huo ulioandikwa kwa mkono ulikuwa umechakaa sana ulikabidhiwa  kwa Mwalimu Cheng Yen, mwanzilishi wa Taasisi ya Kibudha ya Tzu Chi yenye makao yake Taiwan, kama zawadi mwaka wa 2020 na Faisal Hu, mfanyakazi wa kujitolea wa Tzu Chi na Muislamu anayeishi Uturuki.
Hata hivyo, Cheng Yen  aina ya mdudu anayepatikana sana katika vitabu vya zamani -- kwenye Msahafu huo na akaelekea Maktaba ya Kitaifa ya Taiwan kwa usaidizi kupitia Hu na mfanyakazi mwingine wa kujitolea Wu Ying-mei, ambaye alikuwa naibu mkurugenzi wa maktaba ya wakati, maktaba ilisema.
Marejesho hayo yalichukua muda wa miezi 35, ikijumuisha kusitishwa shughuli hiyo kwa takriban mwaka mmoja na nusu kutokana na janga la COVID-19, kabla ya Hu, mkurugenzi wa maktaba Tsao Tsui-ying na warejeshaji katika maktaba kuwasilisha kazi iliyorejeshwa kwa Cheng Yen huko Hualien mnamo Jumatatu.
Huo ndio Msahafu mkongwe zaidi kurejeshwa na maktaba hiyo, kulingana na Tsao, ambaye alisema urejeshaji wa mafanikio wa maandishi ya kidini una umuhimu wa kihistoria na ni utambuzi wa taaluma na utaalamu wa timu yake.

5-Centuries-Old Quran Restored in Taiwan

Kishikizo: taiwan msahafu kale
captcha