IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu / 82

Surah Al-Infitar; Hatima ya wale wasiokuwa na shukrani kwa Mwenyezi Mungu

20:19 - June 06, 2023
Habari ID: 3477107
Mwanadamu ana baraka nyingi maishani, ambazo zote amepewa na Mwenyezi Mungu. Lakini wakati mwingine anazichukulia kuwa za kawaida na kushindwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema alizomtunuku.

Hatima ya watu hao wasio na shukrani imejadiliwa katika Surah Al-Infitar ya Qur'ani Tukufu. Al-Infitar ni jina la sura ya 82 ya Qur'ani Tukufu, ambayo ina aya 19 na iko katika Juzuu ya 30. Ni Makki na ni Sura ya 82 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Infitar maana yake ni kugawanyika na kupasuliwa na katika Sura hii inahusu kupasuka mbingu na kila kitu katika anga za mbali  kabla ya Siku ya Kiyama. Hivi ndivyo aya ya kwanza inazungumzia na hivyo jina la sura.

Sura inahusu Siku ya Kiyama, ishara zake, jinsi inavyotokea na hatima ya Abrar (wafanyao wema) na Fujjar (wadhalimu) siku hiyo.

Abrar hupokea baraka za Mwenyezi Mungu Siku ya Hukumu na Fujjar huishia kwenye moto wa Jahannam.

Sura ya Al-Infitar inavuta mazingatio ya mwanadamu kwenye baraka za Mwenyezi Mungu alizopewa na kumuuliza jinsi anavyozipuuza na kubaki asiye na shukrani.

Miongoni mwa Aya kuu za Sura ni Aya ya 6 inayosema: “Ewe mwanadamu! Ni nini kimekudanganya juu ya Mola wako Mkarimu?”

Ni juu ya wale walio na majivuno na kusahau kuhusu baraka nyingi walizopewa na Mwenyezi Mungu. Aya inataka kuwaamsha watu na kuwausia wale walioghafilika na wasio na shukrani. Kwa mujibu wa Hadith, Mtukufu Mtume Muhammad (SAW), baada ya kusoma aya hii, alisema kwamba ujinga wa mtu ndio chanzo kikuu cha udanganyifu na majivuno yake.

 

captcha