IQNA

Al-Masjid an-Nabawī

Zaidi ya waumini milioni 200 wametembelea Msikiti wa Mtume SAW katika mwaka huu wa Kiislamu

22:22 - May 30, 2023
Habari ID: 3477072
TEHRAN (IQNA) – Msikiti wa Mtume (Al-Masjid an-Nabawī ) huko Madina, ni mojawapo ya maeneo takatifu zaidi katika Uislamu, na umetembelewa na waumini zaidi ya milioni 200 tangu mwanzo wa mwaka huu wa Kiislamu. Hayo yamedokezwa na Urais Mkuu wa Masuala ya Misikiti Miwili Mitakatifu. .

Mwaka wa Kiislamu, unaojulikana pia kama mwaka wa Hijri, unafuata kalenda ya mwezi ambayo ina miezi kumi na mbili. Mwaka wa sasa ni 1444 AH, ambao ulianza Julai 30, 2022 utamalizika Julai 18, 2023.
Ofisi ya Urais Mkuu wa Masuala ya Misikiti Miwili Mitakatifu imesema kuwa imetoa huduma na vifaa kwa waabudu waliokuja kwenye Msikiti wa Mtume kuswali na kutembelea kaburi la Mtume Muhammad (SAW).
Msikiti huo uliojengwa na Mtume Muhammad (SAW) mwenyewe una uwezo wa kubeba waumini zaidi ya milioni moja na uko katika eneo la takriban mita za mraba 400,000 na una minara kumi na kuba 27. Pia una maktaba, jumba la makumbusho, na hospitali.
Idadi ya waumini katika Msikiti wa Mtume (SAW) inatarajiwa kuongezeka kwa kiasi kikubwa katika mwezi ujao, kwani Waislamu kutoka sehemu mbalimbali duniani watamiminika Saudi Arabia kuhiji, ibada ya kila mwaka ya Hija ambayo ni moja ya nguzo tano za Uislamu.
3483762

captcha