IQNA

Kiongozi Muadhamu katika Mkutano na Sultani wa Oman

Iran na Oman zitafaidika kutokana na ushirikiano wa karibu wa pande mbili

18:08 - May 29, 2023
Habari ID: 3477067
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei alisema siku ya Jumatatu kuwa Iran na Oman zitanufaika kutokana na ushirikiano wa karibu wa pande mbili.

Ayatullah Khamenei ameyasema hayo jijini Tehran katika mkutano wake na Sultan Haitham bin Tariq Al Said wa Oman mjini Tehran. "Tunaamini kwamba upanuzi wa uhusiano wa nchi mbili katika nyanja zote unanufaisha pande zote mbili," Kiongozi Muadhamu alisema. "Kuongezeka kwa ushirikiano wa Iran na Oman ni muhimu kwa sababu nchi hizo mbili zinashiriki Mlango-Bahari wa Hormuz muhimu sana."

Akirejelea mazungumzo kati ya Wairani na Oman, Ayatullah Khamenei alibainisha kuwa mazungumzo hayo yanapaswa kufuatiliwa kwa umakini hadi yatakapotoa matokeo yanayoonekana.

Kiongozi Muadhamu aidha amezitaka nchi zote za eneo kuzingatia siasa zinazofuatwa na utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wake za kuzusha hitilafu na kudidimiza amani katika eneo hili.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, aidha amesema Iran inakaribisha azma ya kufufuliwa uhusiano wake na Misri. Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo katika mazungumzo yake na Sultan. "Tunakaribisha msimamo huu, na hatuoni tatizo katika (kufikiwa) hilo." Kiongozi Muadhamu amesema hayo baada ya kupokea ujumbe wa Misri wa kutaka kufufua uhusiano na Iran uliowasilishwa na Sultan wa Oman.Ameipongeza serikali ya awamu ya 13 ya Jamhuri ya Kiislamu inayoongozwa na Rais Ebrahim Raisi, kwa siasa zake za nje zenye lengo la kuimarisha uhusiano na mataifa ya kieneo.

Kadhalika ameeleza bayana kuwa, kuimarishwa ushirikiano wa Tehran na Muscat kuna umuhimu mkubwa kwa kuwa nchi mbili hizi zina hisa katika mkondo wa maji wa Lango Bahari la Hormuz.

Kwengineko katika matamshi yake, Ayatullah Ali Khamenei ametahadharisha juu ya uwepo wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo. "Lengo la utawala wa Kizayuni ni kuibua migawanyiko na ukosefu wa usalama katika eneo," amesema Kiongozi Muadhamu.

Kuhusiana na kuridhishwa kwa Sultani wa Oman na kurejea tena uhusiano wa Iran na Saudi Arabia, Kiongozi Muadhamu amesema: "Masuala haya ni matokeo ya sera nzuri ya utawala wa Raisi ya kuendeleza na kuimarisha uhusiano na majirani na mataifa ya eneo."

Ayatullah Khamenei ameeleza matumaini yake kuwa Umma wa Kiislamu utarejesha adhama yake kupitia upanuzi wa uhusiano kati ya serikali za eneo, kwani muungano wa uwezo na suhula za nchi za Kiislamu utanufaisha mataifa na serikali zote za Kiislamu.

Kwa upande wake, Sultan Haitham bin Tariq Aal Saeed wa Oman ameeleza kuridhishwa kwake na mkutano wake na Kiongozi Muadhamu na kusema kuwa, nchi yake ina sera ya kuboresha uhusiano na majirani, haswa Jamhuri ya Kiislamu.

Sultan Haitham amesema, "Katika mazungumzo mbalimbali tuliyofanya hapa Tehran, tumejadili kuhusu kuimarisha ushirikiano katika nyuga tofauti." Amesema anatumai kwamba, kwa kuendeleza mazungumzo hayo, Iran na Oman zitaweza kupanua zaidi mahusiano yao.

Sultan wa Oman ameondoka nchini baada ya kuonana na Kiongozi Muadhamu. Alikuwa ameandamana na ujumbe wa ngazi za juu katika ziara hiyo rasmi ya siku mbili hapa Tehran.

4144356

Habari zinazohusiana
captcha