IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Wizara ya Mafunzo ni mlezi na muandaji wa kizazi chenye kujenga ustaarabu wa Kiislamu-Kiirani

22:11 - May 11, 2022
Habari ID: 3475237
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, Wizara ya Mafunzo na Malezi ni mlezi na muandaji wa kizazi chenye kujenga ustaarabu.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema hayo leo alipokutana na mamia ya walimu wa Iran na kubainisha kwamba, kizazi cha mabarobaro na vijana kinapaswa kuwa na utambulisho wa Kiislamu-Kiirani chenye sifa za kujiamini, kusimama kidete, weledi wa fikra za Imam Khomeini MA na malengo matukufu, usomi na chenye manufaa.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiiislamu ameashiria malengo ya muda mrefu ya kuleta ustaarabu wa kisasa na wenye ustawi wa Kiislamu na kueleza bayana kwamba, watu wanahesabiwa kuwa miundombinu ya kila ustaarabu na wasimamishaji wa ustaarabu mpya wa Kiislamu ambao kwa sasa wako chini ya walimu.

Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa, kwa kuzingatia hayo, inapaswa kutambua umuhimu na thamani ya mwalimu katika engo hii.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amebainisha kwamba, kudiriki thamani ya kusimama kidete na kutotetereka ni miongoni mwa mahitaji ya wanafunzi na kuongeza kuwa, katika ulimwengu ambao kila mtu iwe ni Magharibi au Mashariki anatumia lugha ya mabavu, kizazi kijacho kinapaswa kujifunza kuanzia sasa thamani na umuhimu wa kusimama kidete ili kupitia mafundisho hayo kiwe ni chenye ustaarabu na hivyo kije na kujenga taifa na nchi ambayo ina izza na heshima.

4056236/

captcha