IQNA

Mwanamke Mpalestina aliyeandika tafsiri ya Qur’ani Tukufu

13:41 - January 25, 2022
Habari ID: 3474849
TEHRAN (IQNA)- Naila Sabri ni mwanamke Mpalestina ambaye ameandika Tafsiri ya Qur’ani Tukufu ijulikanayo kama Tafsir al-Mubsir li-Nur al-Quran na hatua yake hiyo imepongezwa kuwa ni mafanikio makubwa kwa Wapalestina.

Naila alizaliwa mwaka 1944 katika mji wa Qalqilya katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan katika familia ya kidini. Baba yake mzazi alihitimu katika Chuo Kikuu cha Al Azhar Misri na alihudumu kama Mufti wa Qalqilya kwa miaka kadhaa.

Naila aliingia katika chuo kikuu cha Kiislamu baada ya kumaliza shule ya upili. Alipohitimu alitumia muda wa miaka 20 kuandika tafsiri yake ya Qur’ani Tukufu. Katika kipindi hicho alisoma tafsiri 150 za Qur’ani Tukufu, vitabu vingi vya Hadithi za Mtume SAW na maudhui zingine muhimu. Tafsir al-Mubsir li-Nur al-Quran yenye jildi 10 ilichapishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1997 katika Umoja wa Falme za Kiarabu na chapa ya mwili ya mwaka 2003 ilikuwa nchini Bahrain.

Hivi sasa Naila anafunza dini katika Msikiti Mtakatifu wa Al Aqsa mjini Quds (Jerusalem) na amewahi kushiriki katika warsha za Qur’ani katika nchi mbali mbali za dunia kama vile Norway, Sweden, Ufaransa, Marekani, Canada, Afrika Kusini, Uingereza, Uswisi, Uturuki, Ujerumani, Denmark, India, Korea Kusini, Brazil na Romania.

Mume wa Naila ni Sheikh Ekrima Sabri, imamu wa Msikiti wa Al Aqsa ambaye aliwahi kuwa Mufti wa Quds na Palestina. Naila anasema aliolewa akiwaa umri mdogo lakini hali halikumzuia kuendelea na masomo na utaifti wake. Mafanikio ya Naila ni mfano wa wazi kuwa mwanamke anaweza kuwa mama na mke na pia awe msomi wa ngazi za juu na apata mafnaikio makubwa maishani.

A Palestinian Woman Who Studied 150 Quran Interpretations to Write Her Own

A Palestinian Woman Who Studied 150 Quran Interpretations to Write Her Own

A Palestinian Woman Who Studied 150 Quran Interpretations to Write Her Own

4031030

captcha