IQNA

China yawapa chanjo ya bure ya corona wakimbizi Warohingya

15:58 - January 20, 2021
Habari ID: 3473574
TEHRAN (IQNA) – China imesema itatoa chanjo ya bure ya COVID-19 kwa wakimbizi Warohingya ambao walioko Bangladesh.

Kwamujibu wa taarifa chanjo hiyo watapata wale ambao wako katika kundi la kwanza la wakimbizi watakaorejeshwa makwao nchini Myanmar.

Imedokezwa kuwa Myanmar imeafiki mapatano ya pande tatu ya China, Bangladesh na Myanmar kuhusu kuanza kurejeshwa nyumbani wakimbizi Warohingya. Bangladesh imetangaza kuwa tayari kuanza kutekeleza mpango huo lakini Myanmar imekuwa ikiukahirisha.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Bangladesh Masud Bin Momen anasema kurejeshwa nyumbani ndio njia pekee ya kutatoa mgogoro wa jamii ya Warohingya.

Itakumbukwa kuwa wimbi jipya la mauaji, mashambulizi na ubakaji wa jeshi la Myanmar katika mkoa wa Rakhine kuwalenga Waislamu wa Rohingya, lilianza tarehe 25 Agosti mwaka 2017 ambapo zaidi ya Waislamu elfu sita waliuawa na wengine elfu nane kujeruhiwa. Aidha zaidi ya Waislamu wengine milioni moja wa jamii hiyo walilazimika kukimbilia nchi jirani ya Bangladesh huku wengine wakipata hifadhi katika nchi kama vile India, Thailand na Malaysia.

Aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein aliesema kuwa uhalifu unaofanywa na Mabudha kwa himaya ya serikali nchini Myanmar dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya ni mauaji ya kimbari.

Mwezi Januari mwaka huu, Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ) iliitaka serikali ya Myanmar kuchukua hatua za dharura za kuzuia mauaji ya kimbari ya Waislamu wa Rohingya, ikisisitiza kuwa Warohingya hao wamesababishiwa machungu na maumivu yasiyoweza kufutika au kurekebishika.

3948916

Kishikizo: rohingya waislamu chanjo
captcha