IQNA

Kumbukumbu ya kufa shahidi Bibi Fatima Zahra SA yafanyika Najaf, Iraq

20:08 - January 17, 2021
Habari ID: 3473566
TEHRAN (IQNA) – Maelfu ya wapenzi wa Ahul Bayt wa Mtume SAW wamefika katika mji mtakatifu wa Najaf, Iraq katika maombolezo yaliyofanyika kwa mnasaba wa kukumbuka kufa shahidi Bibi Fatima Zahra SA.

Maombolezo hayo yamefanyika katika Haram Takatifu ya Imam Ali AS.

Katika siku kama ya leo miaka 1431 iliyopita, yaani tarehe 3 Jumada Thani mwaka wa 11 hijria, Bibi Fatimatu-Zahra SA, binti kipenzi cha Bwana Mtume Muhammad SAW na mke wa Imam Ali bin Abi Talib AS alikufa shahidi baada ya kuishi umri mfupi tu lakini uliojaa baraka. Ilikuwa ni katika mwaka wa tano tangu Nabii Muhammad SAW alipobaathiwa na kupewa Utume, wakati mke wake mtukufu Bibi Khadija alipojifungua mtoto wa kike; na Bwana Mtume akampa mwanawe huyo jina la Fatima. Bibi huyo mtukufu alipata maarifa na utambuzi wa mafundisho aali ya mbinguni kupitia malezi aliyopata kwa baba yake, yaani Mtume SAW. Ni kutokana na malezi hayo na kwa kukulia kwenye nyumba ya wahyi, Fatima AS alifikia daraja za juu kabisa za ukamilifu na umaanawi. Bibi huyo mtukufu alikuwa mmoja wa waja wenye hadhi maalum mbele ya Allah, aliyeteka lulu nyingi za ujuzi wa mambo kwenye chemchemi ya elimu za mbinguni. Katika maisha yake yote, Fatimatu-Zahra AS, alikuwa dhihirisho bora la ukarimu na kujitolea, subira na uvumilivu, ukinaifu na kutosheka, taqwa na ukithirishaji wa ibada na utoaji misaada kwa wahitaji. Alikuwa pia mama bora aliyawalea na kuwakuza shakhsia wakubwa wa historia kama Imam Hassan na Imam Hussein AS. Tunatoa mkono wa pole kwa mnasaba wa kukumbuka siku aliyokufa shahidi Bibi Fatimatu-Zahra AS na tunanukuu hapa moja ya lulu za elimu na maarifa zilizotoka kwenye kinywa cha mtukufu huyo. Bibi Fatima amesema: "Yeyote anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Kiyama, inapasa aseme maneno mazuri au anyamaze kimya, kwa sababu Mwenyezi Mungu anawapenda watu wafanyao mema, wenye subira na wasafi wa nyoyo na hawapendi watu wenye ndimi chafu na wanaojipendekeza."

تصاویری از حرم علوی در سالروز شهادت حضرت فاطم(س)

3948215

Kishikizo: fatima zahra as
captcha