IQNA

Waislamu Uingereza watoa msaada wakati wa corona

20:12 - January 14, 2021
Habari ID: 3473557
TEHRAN (IQNA) – Waislamu nchini Uingereza wanatoa msaada kwa mamia ya watu ambao wamekumbwa na matatizo ya kumudu mahitaji ya kimaisha katika kipindi hiki cha janga la COVID-19 au corona nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa, Taasisi ya Al-Khair imekuwa ikifanya kazi usiku na mchana kutayarisha vifurushi vya chakula kwa ajili ya watu wasio na uwezo wa kupata chakula.

Familia ambazo zinahitaji misaada zimetambuliwa na Baraza la Mji wa Croydon kusini mwa London na aghalabu ya wanaosaidiwa ni wale ambao hawajiwezi baada ya kufutwa kazi  n.k.

Kati ya vyakula wanavyopata ni mchele, mchuzi wa ndengu na pasta na chakula hicho kinawafikia wenye kuhitaji kikiwa moto kwa kuzingatia sasa ni msimu wa baridi kali nchini Uingereza.

Mkuu wa miradi maalumu katika Taasisi ya Al-Khair, Imran Nisar anasema katika nyakati hizi ngumu wataendelea kuunga mkono familia zisizojiweza. Anasema maombi ya misaada yanazidi kuongezeka huku sheria za kutotoka nje zikiendelea kutekelezwa ili kuzuia maambukizi ya corona. Amesema idadi kubwa ya watu wana hatari ya kufukizwa katika nyumba wanamooshi baada ya kufutiwa kazi kutokana na janga la corona na hivyo itakuwa vigumu kwao kulisha familia zao.

Taasisi ya Al Khair ina matawi kote Uingereza na imekuwa ikitoa misaada ya chakula kwa watu wengi ambao hawana uwezo. Aidha katika uga wa kimataifa, hadi kuanzishwa kwake, Al Khair imetoa misaada yenye thamani ya pauni 195 kwa watu wasiojiweza kwa kuwapa huduma za afya, maji, elimu, ajira, chakula na makazi.

Hadi kufikia 14 Januari watu ambao wameambukizwa corona nchini Uingereza ni zaidi ya milioni 3.21 huku waliofariki wakipindukia 85,000. Jumanne wiki hii imevunja rekodi  kwani watu zaidi ya 1,564 wamepoteza maisha kutokana na corona katika kipindi cha siku moja kote Uingereza. Hali hiyo imepelekea serikali itekeleze sheria kali za kuwazuia watu kutoka nje huku mashirika mengi yakilazimika kuwafuta kazi watu wengi kutokana na biashara kupungua kwa kiasi kikubwa.

3473696

captcha