IQNA

Qiraa ya Qur'ani ya Qari Ragheb Mustafa Ghalwash katika televisheni ya Iran

20:29 - January 12, 2021
Habari ID: 3473551
TEHRAN (IQNA) - Televisheni ya Qur’ani ya Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) imerusha hewnai qiraa ya qarii mashuhuri wa Misri Sheikh Ragheb Mustafa Ghalwash.

Katika klipu hiyo, qarii huyo maarufu wa Misri anasema aya za Sura An-Naba, At-Tariq na Al-Alaq.

Sheikh Ragheb Mustafa Ghalwash  alizaliwa Julai 5 mwaka 1938 nchini Misri na kukulia katika familia iliyokuwa na mapenzi makubwa na Qur'ani. Raghib Mustafa Ghalwash alikuwa tayari amehifadhi Qur'ani nzima katika rika la ubalobaro na kuanza kusoma kitabu hicho katika hafali na majlisi mbalimbali akiwa na umri wa miaka 16. Sheikh Raghib Mustafa Ghalwash alikuwa miongoni mwa wasomaji wa Qur'ani waliofanya safari nchini Iran baada ya kumalizika vita vya kulazimishwa vilivyoanzisha na Iraq dhidi ya Iran. Sheikh Ghalwash aliaga dunia Februari 4 mwaka 2016 akiwa na umri wa miaka 77 uliojaa baraka.

Qiraa na kisomo cha gwiji huyo wa Misri kilipendwa sana nchini Iran. 

Sheikh Ghalwash alitembelea Iran nyakati tafauti kuanzia mwaka 1989 hadi 2000 na katika moja ya safari zake hizo alipata fursa ya kusoma Qur’ani Tukufu katika kikao kilichohudhuriwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyed Ali Khamenei.

3946942

captcha