IQNA

Uwahhabi wajipenyeza Afrika kukabiliana na ushawishi wa nchi zingine za Kiislamu

11:40 - January 04, 2021
Habari ID: 3473522
TEHRAN (IQNA) – Uwekezaji wa Saudi Arabia katika uga wa utamaduni na kidini miongoni mwa jamii za Waislamu umekithiri katika bara la Afrika kwa lengo la kuzuia ushawishi brani humo wa madola makubwa ya Kiislamu kama vile Uturuki na Iran.

Saudia inatumia kila mbinu kueneza itikadi yake rasmi ya Uwahhabi katika nchi za Afrika mbali na kujaribu kuimarisha satwa yake ya kisiasa, kiuchumi na kiusalama katika bara hilo

Hivi sasa bara la Afrika ni eneo kubwa zaidi lenye uwezo wa uwekezaji kiuchumi duniani na kwa msingi huo madola mengine makubwa duniani kama vile China na Marekani na halikadhalika madola ya Umoja Ulaya yamejikita katika uwekezaji barani Afrika.

Saudia nayo sasa inajaribu kutumia fursa ya ukuruba wa kidini na kijiografia na pia utumizi wa lugha ya Kiarabu katika nchi za kaskazini na mashariki mwa Afrika kujipenyeza zaidi katika bara hilo.

Saudia inawekeza katika sekta za kiutamaduni na kidini barani Afrika kwa kuzingatia idadi kubwa ya Waislamu barani humo na inafanya hivyo kuzuia ushawishi wa madola mengine makubwa ya ulimwengu wa Kiislamu barani humo kama vile Iran na Uturuki. Ili kukabiliana na madola hayo mawili Saudia inaeneza itikadi ya Uwahabbi ambayo haistahamili Waislamu wenye fikra zingine.

Moja ya mbinu ambayo Saudia imekuwa ikitumia kueneza Uwahhabi Afrika ni kuwapa msaada wa masomo Waafrika kuelekea Saudia kusoma katika vyuo vikuu vya Madina na Riyadh. Hivi sasa maelfu ya maimamu na wahubiri wa kidini Waafrika wamehitimu kutoka vyuo hivyo vikuu.

Aidha katika uga wa kijamii taasisi za Saudia zimekuwa zikijipenyeza Afrika kwa kutoa misaada ya mabilioni ya dola ili kuwavutia wafuasi.

Katika uga wa kisiasa pia Saudia imeweza kujipenyeza katika nchi nyingi za Kiafrika na kuziharibia jina nchi za Kiislamu duniani ambazo hazikubaliani na Uwahabbi. Kwa mfano Saudia imekuwa ikieneza propaganda chafu kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni nembo ya utawala wa Kishia nayo Uturuki imekuwa ikitajwa kwama nembo ya Uislamu wa Kisekula huku Indonesia na Malaysia zikiarifishwa kama nchi ambazo zimekumbatia mfumo wa kisasa kwa madhara ya Uislamu.

Matokeo ya propaganda hizo za Saudia imekuwa ni nchi kadhaa za Kiafrika kama vile Sudan, Comoro, na Djibouti kukata uhusiano na Iran baada ya matukio katika ubalozi wa Saudia mjini Tehran miaka kadhaa iliyopita. Aidha baadhi ya nchi za Kiafrika zimekata uhusiano na Qatar kufuatia mgogoro unaoendelea baina ya Saudia na Qatar.

Pamoja na kuwa Saudia imewekeza sana barani Afrika ili kubadili fikra za waliowengi hasa Waislamu, lakini watu wa Afrika wanafahamu kuwa Saudia imekuwa na sera haribifu barani humo. Mfano wa wazi ni ungaji mkono wa Saudia kwa utawala wa kijeshi Misri baada ya mapinduzi ya wananchi yaliyopelekea Hosni Mubarak aondolewe madarakani. Aidha Saudia iliunga mkono dikteta aliyetimiliwa madarakni Tunisia na hivi sasa Saudia pia inamuunga mkono Jenerali muasi Khalifa Haftar ambaye amekuwa akitekeleza jina Libya.

Aidha kufuatia mapinduzi ya wananchi wa Sudan ambayo yalipelekea kutimuliwa madarakani dikteta Omar al Bashir aliyetawala nchi hiyo kwa muda wa miaka 30, Saudia iliunga mkono wanajeshi ambao waliyateka mapinduzi hayo.

Uenezaji wa itikadi ya Uwahhabi Afrika umeandamana na kuibuka makundi ya kigaidi yenye kufuatia itikadi hiyo kali. Makundi hayo Kiwahhabi ambayo yameenza wahka na hofu barani Afrika mbali na kuuharibia jinai Uislamu ni kama vile Al Shabab na Boko Haram. Kwa msingi hiyo Waislamu barani Afrika wanadiriki hali ya mambo lakini na sasa wanakabiliana na vikra za  Uwahhabi wa Saudia ambao umepelekea usalama kukosekana katika maeneo mengi barani humo.

3945404

Kishikizo: uwahhabi saudia afrika
captcha