IQNA

Jumuiya ya Maulama wa Kiislamu Duniani

Kuanzisha uhusiano na Israel ni haramu kwa mujibu wa sheria za Kiislamu

22:06 - December 28, 2020
Habari ID: 3473502
TEHRAN (IQNA)- Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa Waislamu (IAMS) amesema kuwa, viongozi wanaotaka mapatano wameanzisha uhusiano wa kawaida na Israel kwa sababu ya woga, tamaa na kwa ajili ya kulinda maslahi yao pamoja na tawala zao, hatua ambayo ni haramu na batili.

Mwenyekiti wa jumuiya hiyoa Sheikh Ahmad al-Raysuni amesema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na mtandao wa Palestina wa Quds Press na kueleza kwamba, maulamaa Waislamu daima ni waungaji mkono wa haki za Wapalestina na daima kadhia ya Quds ndio jambo linalozingatiwa na wasomi hao.

Dakta al-Raysuni kadhalika amesema kwamba, Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa Waislamu haitaacha kuunga mkono kufanyika mikutano, makongamano na harakati mbalimbali kwa ajili ya kuiunga mkono kadhia ya Palestina na daima inapinga hatua yoyote ile yenye lengo la kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.

Vilevile Sheikh Ahmad al-Raysuni amebainisha kwamba, Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa Waislamu hadi sasa imetoa taarifa kadhaa ikitangaza wazi kwamba, kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Israel ni haramu na batili.

Hivi karibuni Morocco na utawala wa Kizayuni wa Israel zilianzisha uhusiano wa kawaida kati yao kufuatia mashinikizo ya kila upande ya rais wa Marekani, Donald Trump.

Uamuzi huo wa Morocco kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel unafuatia uamuazi sawa na huo uliochukuliwa miezi ya karibuni na Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain na Sudan. Nchi zingine za Kiarabu ambazo zina uhusiano rasmi na utawala bandia wa Israel ni Misri na Jordan.

Hatua ya madola hayo ya Kiarabu kuanzisha uhusiano na Israel inaendelea kulaaniwa kote duniani na kutajwa kuwa ni usaliti kwa harakati za kupigania ukombozi wa ardhi za Palestina zinazokoloniwa na Israel.

3944019

Kishikizo: israel palestina morocco
captcha