IQNA

Rais wa ya Iran katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria

Kukabiliana Wazayuni na ugaidi ni lengo la pamoja la mataifa mawili ya Iran na Syria

20:48 - December 08, 2020
Habari ID: 3473435
TEHRAN (IQNA) - Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesemam kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendeleza maamuzi na irada ambayo imekuwa ikichukua katika kuiunga mkono serikali na taifa la Syria kama nchi muitifakii wake wa kistratejia na itakuwa bega kwa bega na Syria hadi kupatikana ushindi wa mwisho.

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo Jumanne amekutana na kufanya mazungumzo hapa Tehran na Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Feisal Mekdad na kusisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran siku zote iko pamoja na wananchi na serikali ya Syria. Rais Rouhani aidha amebainisha kuwa kukabiliana na maghasibu wa Kizayuni na ugaidi ni lengo la pamoja la mataifa mawili ya Iran na Syria.  

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Iran itaendelea kuwa pamoja na Syria katika upande wa kisiasa; na katika uwanja huo inaamini kuwa mchakato wa Astana unatekelezwa kwa ajili ya kulinda maslahi na umoja wa ardhi nzima ya Syria na inafuatilia kwa dhati suala hilo.   

Katika mazungumzo hayo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria hapa Tehran, Rais Rouhani ameashiria pia hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kuunganisha sehemu ya ardhi ya Syria na ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na adui Mzayuni na kueleza kuwa tunapasa kukabiliana na maghasibu wa Kizayuni ili kukomboa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu ikiwemo miinuko ya Golan. 

Rais Rouhani amesisitiza kuendelezwa muqawama na kukabiliana vilivyo mataifa ya eneo  na ugaidi na vitendo vya uvamizi. Rais wa Iran ameashiria kuuliwa shahidi Kamanda Suleimani na Shahidi Fakhrizadeh na kueleza kuwa lengo la maadui kumuua shahidi Kamanda Suleimani halikuwa tu kulipiza kisasi kwa muqawama wa taifa la Iran bali kulipiza kisasi kwa mataifa mengine ya eneo; na maadui wanataka pia kulipiza kisasi kwa suala zima la maendeleo ya sayansi na teknolojia kwa kumuua shahidi Fakhrizadeh. 

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria ametoa mkono wa pole kufuatia kuuliwa shahidi Mohsen Fakhrizadeh na Kamanda Suleimani na kueleza kuwa; yoyote anayetenda jinai kama hizo hajui kwamba kumwaga damu za mashahidi wa mataifa ya eneo kunaongezeka tu ari yao ya kufikia ushindi. 

3939818

 

captcha