IQNA

Madaktari kutoka nchi 10 wanawahudumia wafanyaziara katika Arubaini ya Imam Hussein

10:38 - October 17, 2019
Habari ID: 3472175
TEHRAN (IQNA) –Madaktari wa kujitolea kutoka nchi 10 wanatoa huduma za kitiba bila malipo kwa wafnyaziara katika Arubaini ya Imam Hussein AS nchini Iraq.

Ahmed Jalil al Shimri, mkurugenzi wa vituo vya kitiba katika Idara ya Mfawidhi wa Haram ya Imam Hussein AS amesema madaktari wanaotoa huduma bila malipo ni kutoka nchi za Iraq, Australia, Tanzania, India, Pakistan, Bahrain, Saudi Arabia, Kuwait, Lebanon na Syria.

Ameongeza kuwa idara hiyo ina vituo 35 vya kitiba Karbala na vituo tatu vya huduma za tiba katika barabara zinazoelekea katika mji huo mtakatifu. Al Shimri amesema huduma za afya zitatolewa kwa masaa 24.

Inafaa kuashiria hapa kuwa, tarehe 20 Safar inasadifiana na kutimia Arubaini ya kuuawa shahidi Mjukuu wa Mtume Muhammad SAW,  Imam Hussein AS pamoja na wafuasi wake 72. Imam Husain AS aliuawa shahidi kikatili na kinyama tarehe 10 Muharram mwaka wa 61 Hijria, yaani miaka 1380 iliyopita, katika jangwa la Karbala, Iraq ya leo, akiwa na umri wa miaka 57 baada ya kuongoza mapambano ya kishujaa ya ushindi wa damu mbele ya upanga.

Vita vya Karbala vilikuwa moja kati ya vita mashuhuri katika historia ya Kiislamu na ya mwanadamu, vilitokea baina ya majeshi ya haki na batili katika ardhi ya Karbala huko Iraq. Siku aliyouawa shahidi Imam Hussein AS inajulikana kwa jina la Ashura.

Mwaka huu Siku ya Arubaini itakuwa Oktoba 19 na wafanyaziara zaidi ya milioni 20 wanatazamiwa kushiriki katika matembezi ya siku hiyo.

3469679

captcha