IQNA

Maafisa wa polisi wa kike Waislamu Uingereza wapata sare zenye hijabu

16:42 - September 19, 2018
Habari ID: 3471679
TEHRAN (IQNA)- Polisi katika eneo la West Yorkshire Uingereza wamezindua sare ya maafisa wa kike Waislamu ambayo inazingatia mafundisho ya Kiislamu ya mavazi yaliyo na staha.

Sare hiyo mpya haitawabana maafisa wanawake na pia inajumuisha mtandio kichwani na hivyo kuwawezesha maafisa wa kike ambao ni Waislamu kufanya kazi zao kwa kuzingatia mafundisho ya Kiislamu. Idara ya polisis imesema lengo la mabadiliko hayo ni kuwapa fursa wanawake Waislamu kuhudumu kama maafisa wa polisi. Tayari mtandio hutumiwa na maafisa wanawake Waislamu katika kikosi cha polisi kote Uingereza.

Firzana Ahmed ambaye alikuwa afisa wa kwanza wa kike Mwislamu kuvaa sare hiyo mpya amesema Waislamu wa eneo la Bradford wamepongeza uamuzi wa Idara ya Polisi kuhusu hijabu.

Afisa mwandamizi wa polisi Dee Collins amesema kumekuwa na wasiwasi kuwa mavazi yenye kuwabana maafisa wanawake ni moja ya sababu ambazo zimepelekea wanawake Waislamu wasijiunge na kikosi cha polisi.

Kwa mujibu wa sensa ya hivi karibuni ya watu Uingereza, kuna Waislamu milioni 2.8 nchini humo kati ya watu milioni 64 nchini humo. Waislamu wameenea katika maeneo yote ya Uingereza na wamewakilishwa katika sekta zote za kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni.

3748268

captcha