IQNA

Mmarekani aibuka Mshindi wa Mashindano ya Qur’ani Dubai

13:22 - June 06, 2018
Habari ID: 3471545
TEHRAN (IQNA)- Mmarekani Ahmad Burhan ametangazwa mshindani wa Mashindano ya 22 ya Kuhifadhi Qur’ani ya Dubai.

Burhan, mwenye umri wa miaka 16, ametunukiwa zawadi ya Dh 250,000 Jumanne katika sherehe iliyofanyika Jumanne katika ukumbi wa Jumuiya ya Kiutamaduni na Kisayansi ya Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu.

Nafasi ya pili katika mashindano hayo imechukuliwa na Hamzah Al Basheer wa Libya na Mohammad Maarif wa Tunisia ameshika nafasi ya tatu akifuatiwa na Ahmad Herkat wa Algeria.

Hii ni mara ya kwanza kwa mwakilishi wa Marekani kushika nafasi ya kwanza katika mashindano hayo ambao pia yanajulikana kama Zawadi ya Kimataifa ya Dubai (DIHQA). Mashindano ya mwaka huu yaliyofanyika baina ya tarehe 7-20 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani yalikuwa na washiriki 96 kutoka maeneo yote ya dunia.

Mmarekani aibuka Mshindi wa Mashindano ya Qur’ani Dubai

3720659

captcha