Katika taarifa , OIC imesema al-Othaimeen na Papa Francis wamekutana Ijumaa mjini Vatican ambapo walisisitiza kuhusu mazungumzo baina dini huku wakisisitiza kuhusu hekima na kuishi kwa maelewnao ili kukabiliana na misimamo mikali na ugaidi.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, al-Othaimeen amemsisitizia Papa Francis kuwa ugaidi hauna nafasi yoyote katika dini na kwamba OIC inalaani vitendo vyote vya kigaidi kutoka katika dini yoyote.
"Al Othaimeen pia amemshukuru Papa Francis kutokana na msimamo wake kuhusu Quds Tukufu (Jerusalem) na haki za Waislamu na Wakristo katika mji huo mtakatifu."
Aidha Katibu Mkuu wa OIC pia amempongeza papa kwa msimamo wake wa kuunga mkono Waislamu Warohingya wanaokandamizwa Myanmar na wahamiaji.